Exodus 20:2-7

2 a“Mimi ndimi Bwana Mwenyezi Mungu wako, niliyekutoa Misri, kutoka nchi ya utumwa.
3 bUsiwe na miungu mingine ila mimi.
4 cUsijitengenezee sanamu katika umbo la kitu chochote kilicho juu mbinguni, au duniani chini, au ndani ya maji. 5 dUsivisujudie wala kuviabudu; kwa kuwa Mimi, Bwana Mwenyezi Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi za baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 6 elakini ninaonyesha upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanipendao na kuzishika amri zangu.
7 fUsilitaje bure jina la Bwana Mwenyezi Mungu wako, kwa kuwa Bwana hataacha kumhesabia hatia yeye alitajaye jina lake bure.
Copyright information for SwhKC